BETI NASI UTAJIRIKE

MORRISON NA YANGA MAMBO NDIO KWANZA YAMEANZA UPYA


Klabu ya Yanga kupitia Mwenyekiti wake Mshindo Msolla ilisema kuwa MORRISON ni mchezaji wao na wamemjumuisha kwenye kikosi Chao na kesho Jumatatu wanapeleka malalamiko yao rasmi FIFA wakidai kuwa na mkataba halali na winga. Mchezaji Bernard MORRISON kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii ni kama amewapiga dongo Yanga kuwa huko nako hawataambulia kitu. 
Morrison jana alionyesha thamani yake kwa kufunga bao pamoja na kutoa asisti kwenye ushindi wa mabao 6-0 dhidi ya Vital'o ukiwa ni mchezo wa Simba Day. 
Inaelezwa klabu ya Yanga imemjumuisha Morrison kwenye usajili wao, jina lake wakiwa wamelisajili kwenye mfumo wa FIFA (TMS)
Sakata hili linaweza kuwaingiza Yanga wenyewe matatani huko FIFA kama itabainika ni kweli walifoji mkataba huo


Post a Comment

0 Comments