BETI NASI UTAJIRIKE

MKONGWE MASCHIO AWATOFAUTISHA MESSI,PELE NA MARADONA .AMTAJA BABA LAO


Nyota wa zamani aliyewahi kuzitumikia timu za Argentina miaka ya 1957 na kuisaidia timu hiyo kutwaa kombe la Copa America kisha kuisaidia Italy kucheza kombe la Dunia mwaka 1962 Humberto Maschio amefunguka na kusema Lionel Messi ndiye bora zaidi Duniani.

Maschio amesema Messi ni zaidi ya Maradona, Alfredo Di Stefano ,Pele na hata Johan Cruff. Nyota huyo wa zamani amesema

" Nimemuona Cruffy,Pele ,Maradona lakini Messi ni bora zaidi ya wote na alistahili kushinda Ballorn D Or mara 6 . Nimekwishawahi cheza na hawa nyota baadhi na ninakili Messi ni zaidi yao.

Pele na maradona walikuwa bora kwa miaka yao ila mpira wa kisasa ni tofauti kabisa ,hebu jaribu kuangalia  Mabao yanayofungwa na Messi. Leo hakimbii kimbii hovyo uwanjani ila inapobidi hukumbia utadhani mpira umenasa miguuni.

Nimeona wachezaji wengi wenye vipaji wanapokuwa na mpira hupunguza spidi lakini Messi ni tofauti anafanya mambo makubwa tena akiwa na spidi kali.

Messi anazidi kuwa mjadala duniani baada ya kushinda mataji 10 ya La liga na yale manne ya Ligi ya Mabingwa huku akifuga mabao 633 kwenye michezo 729 akiitumikia Barcelona

Nyota huyo amefunga jumla ya mabao 70 kwenye mechi 138 alizoitumikia timu yake ya taifa Argentina . Messi amezidiwa na Pelle na Maradona baada ya nyota hao kushinda makombe ya dunia. Pele akitwaa mara 3 huku Maradona  akitwaa mara 1

Post a Comment

0 Comments