BETI NASI UTAJIRIKE

MENEJA WA PAUL POGBA ATOA HATIMA YA MCHEZAJI HUYO NA MANCHESTER UNITED


Meneja wa Paul Pogba amethibitisha kwamba mchezaji huyo hataondoka Manchester United na kwa sasa timu hiyo inafungua majadiliano ya kimkataba na mchezaji huyo. Mchezaji huyo mwenye miaka 27 alijiunga na Manchester United akitokea Juventus kwa ada ya dola milioni 105 na mkataba wake umebakiza miezi 12 kumalizika huku kukiwa na kipengere cha kumuongezea.

Awali mchezaji huyo alihusiswa na kuondoka klabuni hapo na Real Madrid pamoja na Juventus ni baadhi ya klabu ambazo alipaswa kujiunga nazo. Mchezaji huyo hakusema chochote kuhusiana na tetesi hizo huku akigeuka msaada kwa Manchester United tangu aliporejea kutoka majeruhi na kuifanya timu hiyo ifuzu kucheza ligi ya mabingwa ulaya.

Mino Raiola meneja wa mchezaji huyo amenukuliwa akisema "Yupo kwenye mipango ya kiufundi na Manchester United hawajataka kufungua makubaliano kwa miaka ya karibuni kama atauzwa ama la. Tunafanya mazungumzo yetu kwa ukaribu kabisa bila stresi

Post a Comment

0 Comments