BETI NASI UTAJIRIKE

MBADALA WA JAFFARI APATIKANA YANGA


Klabu ya Yanga imeendelea kuimalisha safu yake ya ulinzi kwa kumsajili beki mpya kutoka Polisi Tanzania Yassin Mustafa. Yassin amekuwa kwenye kiwango kizuri msimu wa 2019/2020 na hicho ni kigezo haswa kilichotumika.

Kwa upande klabu ya Yanga imekuwa na wakati mgumu upande wa kushoto tangu alipoondoka Gadiel Michael kwenda Simba. Makocha wa Yanga wamekuwa wakimtumia mchezaji kiraka Jaffari kukava nafasi hiyo na alifanikiwa kwa kiasi fulani.

Usajili wa Yassin unakuwa na tija kwa mabingwa hao wa kihistoria kuelekea msimu wa 2020/21 ikizingatiwa timu hiyo itashiriki michuano ya kimataifa baada ya kumaliza nafasi ya pili kwa msimu wa 2019/20.

Bado haijawekwa wazi mkataba wa mchezaji huyo na Yanga utadumu kwa muda gani.

Pichani ni Yassin Mustafa akiwa na meneja wa udhamini Eng.Hersi kutoka GSM Post a Comment

0 Comments