BETI NASI UTAJIRIKE

MECHI KALI LEO: JE NANI ATAIBUKA NA UBINGWA WA UEFA LEO


 Kwa mara ya kwanza kikosi cha PSG kimefuzu fainali ya mabingwa ulaya na leo hii kinavaana na Bayern Munich ya ujerumani yenye makombe matano ya michuano hiyo. Mchezo huo unategemewa kuwa mkali kwani timuzote zinawachezaji wa kiwango kikubwa mno.

Bayern Munich wanamtegemea Gnabry,Muller na Lewandowski kwenye kuongoza mashambulizi na kwa pamoja wamefunga jumla ya mabao 41 kwenye mechi 10 za ,michuano hiyo. Robert Lewandowski ndiye kinara wa michuano hiyo akifunga mabao 14.

PSG wanawategemea Neymar,Mbappe na Di Maria wachezaji wenye spidi kubwa zaidi kwa timu za ulaya. PSG imecheza michezo 10 ikishinda 8 sare 1 na kufungwa 1 huku wakifunga mabao 25.

Swali linabaki kwa mashabiki nani ataibuka na ushindi hii leo? Kaa karibu na Amospoti hii leo kuweza kushuhudia uchambuzi makini nitakaoufanya kupitia website yako ya amospoti.com

Post a Comment

0 Comments