BETI NASI UTAJIRIKE

MAKALA:MORRISON ALIVYOMALIZA KUPANDA MPIRA NA SASA ANAWAPANDA VICHWANI AKINA MSOLA NA MWAKALEBELA


Yanga kuachana na nyota wake 14 kwangu hilo si tatizo na nasema ni maamuzi ya kiufundi yaliyofanyika kitaalamu kuelekea Yanga mpya ya kimashindano .Kwa misimu mitatu mfululizo Yanga wamekuwa dhaifu kuanzia ndani ya uwanja mpaka nje ya uwanja .

Hata kwenye vijiwe vya kahawa huwa hatuzungumzii ubora wa Yanga bali migogoro baina ya wachezaji na viongozi kuisimanga Simba na wakati mwingine kuwalaumu viongozi wa bodi ya ligi kuwabania Yanga na kuibeba Simba kitu ambacho si kweli.

Binafsi silidhishwi na maamuzi ya viongozi wa Yanga hasa wanapomwacha mchezaji msumbufu na mtukutu Benard Morrison. Mchezaji huyo amewakataa Yanga hadharani lakini wamemng'ang'ania kwamba anamkataba nao tena wa miaka miwili.

Morrison huyu huyu mechi ya watani aliamua kujiondoa uwanjani maa baada ya kufanyiwa mabadiliko .Tena kwa jeuri akasema hana mkataba na Yanga na ni mchezaji huru , Morrison huyu huyu amewakataa Yanga kupitia vyombo vya habari na kuna kipindi aliwazingua kambini na kutoroka, kuna kipindi alikataa mpaka kusafiri na timu kisa tu alijiskia kutocheza .

Msolla na jopo lake wamemjumuisha tena Bernad Morrison kwenye kikosi cha wachezaji 17 waliobaki Yanga ,hofu yangu ni jinsi wachezaji 16 walivyojiskia baada ya kuona mchezaji msumbufu anabebwa huku wale waliojitolea kwa timu wanatimuliwa.

Nina imani wachezaji wengi wa Yanga watakuwa na nidhamu mbovu kwa msimu wa 2020/21 na hilo litakuwa ni moja ya majibu ya kumbakisha Morrison . Msola na jopo lake wajiandae tena kutukanwa na mashabiki wa Yanga msimu wa 2020/21 kwa matokeo mabovu maana kila mchezaji atafanya anavyojiskia na akiulizwa atasema mbona hamkumalizana na morrison?

Mwisho niseme tu duniani hakuna mchezaji mkubwa zaidi ya timu ila Morrison ni mchezaji mkubwa zaidi ya Yanga na ameshawapanda kichwani viongozi wote wa timu hiyo

Post a Comment

0 Comments