BETI NASI UTAJIRIKE

MAJOGORO ACHUKUA RASMI NAFASI HUMOUD MTIBWA SUGAR


Kiungo mpya wa Mtibwa Sugar Baraka Majogoro amesema kuwa msimu ujao 2020/21 ndani ya Mtibwa Sugar watapambana kufikia malengo ambayo wamejiwekea ili kutoa burudani kwa mashabiki wa timu hiyo.
Msimu wa 2019/20,Mtibwa Sugar ilikuwa kwenye mtikisiko ambapo ilimaliza ikiwa nafasi ya 14 ikiwa na pointi 45 baada ya kucheza mechi 38 jambo ambalo limetokea kwa mara ya kwanza ndani ya misimu 10.
Akizungumza na Championi Jumatatu, kiungo huyo mwenye rasta ambaye alikuwa anakipiga ndani ya  Polisi Tanzania akiwa amesaini dili la miaka miwili alisema kuwa wapo tayari kwa mapambano.

Tupo tayari kwa ajili ya msimu mpya, mashabiki na wadau waendelee kutupa sapoti tutafanya vizuri kwa kuwa tuna malengo na hesabu zetu pia ni kuona kila mmoja anakuwa na furaha kikubwa ushirikiano,mazuri yanakuja,” alisema Majogoro.
 Wengine ambao wametambulishwa ndani ya Mtibwa Sugar ni Abal Kassim Hamisi kiungo mshambuliaji akiwa kwa mkopo kutoka Azam FC na George Makang’a kutoka Namungo naye ni kiungo.

Post a Comment

0 Comments