BETI NASI UTAJIRIKE

MAGORI AFAFANUA MGOGOLO KATI YA YANGA NA MORRISON


Mtendaji wa zamani wa klabu ya Simba Crescentius Magori ambaye kwa sasa ni mshauri wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, amesema Yanga wasitarajie mabadiliko ya maamuzi yaliyotolewa na Kamati ya TFF kuhusu mchezaji Bernard Morrison
Aidha Magori ameitaka klabu hiyo itoe kibali cha Morrison kwani hata wakikizuia TFF watamaliza utata kwa kuweka wazi ni timu ipi imemsajili kihalali
Jana klabu ya Yanga ilidai kukata rufaa Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Michezo (CAS) juu ya uamuzi wa Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF kumtangaza mchezaji huyo kuwa huru baada ya kubaini mapungufu kwenye mkataba wake
"Wamezuia kibali chake lakini hawawezi kumzuia mchezaji kucheza mpira. Shauri lao walilopeleka huko FIFA haliwezi kumzuia Morrison kuitumikia Simba kwa kuwa ni utaratibu wa FIFA kuzingatia maslahi ya mchezaji kwani wakati mwingine shauri linaweza kuchukua muda mrefu"
"Ni wazi wakati shauri hilo likiendelea kusikilizwa Morrison atapewa ruhusa ya kuchagua timu ya kucheza. Iliwahi kutokea kwa Mganda Emmanuel Okwi wakati ana mgogoro na Etoile Du Sahel. Okwi aliruhusiwa kuicheza SC Villa wakati shauri lake likiendelea," alisema Magori
"Lakini pia nawaambia waandike maumivu kwani mchezaji asipokuwa kwenye timu yako huwezi kumpata. Sana sana wanaweza kuambulia kulipwa fidia ya madai kama itatokea wana haki lakini hawawezi kumpata wala kumzuia asicheze mpira"
Kuna taarifa kuwa Yanga imegoma kuachia kibali cha Morrison wakidai kumtambua kuwa mchezaji wao mpaka pale itakapoamuliwa vinginevyo na Mahakama ya CAS

Post a Comment

0 Comments