BETI NASI UTAJIRIKE

MAGOLI AMPA UJUMBE MZITO SENZO


Aliyekuwa mtendaji mkuu wa klabu ya  Simba Crescetius Magori amesema mtu mwenye weledi kama Senzo hatakiwi kuacha kazi kwa kuandika Twitter, alipaswa kufuata taratibu za kuacha kazi ikiwepo kuandika barua rasmi, kukabidhiwa mali za Klabu alizokabidhiwa n.k,

Magori amesema mambo hayo wapaswa wafanye wachezaji sio mtu Kama Senzo,
Kiongozi huyo aliongeza Kuwa yeye ndio aliyehusika kumtafutia Senzo kibali cha kufanya kazi nchini, hivyo pia ili apate kibali kingine cha kufanya kazi pia Simba lazima wahisike

Magoli amenukuliwa akisema "Kwa mtu au kiongozi mwenye weledi PROFESSIONALISM Lazima aandike barua rasmi ya kuacha kazi kwenye Klabu na siyo kuondoka kiholela kwa Kupost kwenye Twitter. (Senzo) Lazima aje akabidhi ofisi na Nyaraka zote za Klabu  pamoja na Asset zote Kama gari aina ya Mercedes Benz n.k. Mambo kama hayo wanafanya wachezaji Ila siyo yeye na hata kibali cha kufanya kazi hapa nchini nilimtafutia mimi kwa haraka hivyo kupata kibali kipya lazima sisi (Simba) tuhusike"


Post a Comment

0 Comments