Klabu ya Simba ni kama imetuma salamu za vitisho kwa timu zote za ligi kuu baada ya kuibua na ushindi wa mabao 6- 0 dhidi ya Vital'o ya Burundi kwenye mchezo wa kirafiki siku ya simba day. Ushindi huo uliambatana na ubora wa wachezaji wote waliosajiliwa msimu huu kuanzia Bernard MORRISON aliyefungua pazia la mabao kwa kufunga dakika ya 45 huku akitengeneza pasi maridadi kwa John Bocco aliyefunga bao la pili dakika za nyongeza kipindi cha kwanza. Beki Onyango alionyesha uwezo wa juu akishirikiana na beki Ibrahim Ame na kufanya safu ya Simba kuwa imara zaidi kwa msimu ujao kwani watakuwa na mabeki watano mahili akiwemo wawa, nyoni, Onyango, Ame na Kennedy. Bwalya naye ameonyesha uwezo mkubwa kwenye mechi hiyo huku Cris Mugalu na Charles Ilanfya wakicheza kwa kiwango kikubwa.
Post a Comment
0
Comments
MERIDIAN BET
EURO 2024
Kuanzia tarehe 14 june to 14 july AMOSPOTIXTRA TEAM itakuwa ujerumani kukuletea michuano ya EURO2024
0 Comments