BETI NASI UTAJIRIKE

KWA MARA YA KWANZA SENZO AFUNGUKA BAADA YA KUSEPA SIMBA


Aliyekuwa mkurugenzi mtendaji wa klabu ya Simba Bw.Senzo Masingisa Mbatha kwa mara ya kwanza amefunguka sababu zilizompelekea kuondoka klabuni hapo. Kwa mujibu wa Senzo amesema klabu hiyo haikuenda sawa na matakwa yake hivyo alilazimika kuondoka. Senzo kwa sasa ni mshauri mkuu wa mwenyekiti mshindo msolla ndani ya Yanga. Senzo amenukuliwa akisema 

Namshukuru Mungu nimewasili salama nchini Tanzania, nikiwa tayari kuanza majukumu yangu! awamu hii nikiwa mwaajiriwa wa Yanga SC.
Kuna jambo acha nitolee ufafanuzi, nimeondoka Simba SC baada ya kuona tunaenda njia tofauti, hata kama isingekuwa Yanga SC pia ningeondoka vilevile. . Naiheshimu sana taaluma yangu kwa maana mpira ndio kazi yangu ndio maana ikanibidi nikae pembeni.
Najisikia vibaya sana kwa mashabiki wa Simba SC walionipenda na kuweka imani kubwa sana kwangu, naomba wanisamehe na wajue kuwa sikudhamiria kuwafedhehesha ama kuwaumiza bali ni sehemu ya maisha.Ntaitumikia klabu yangu ya Yanga SC na kuhakikisha tunafikia malengo yetu"

Post a Comment

0 Comments