advertise with us

ADVERTISE HERE

KUMBE ANAYECHUKUA NAFASI YA JAFARY PALE YANGA AMETOKA NKANA FC


Imeelezwa kwamba Kampuni ya GSM yenye jukumu la kusajili wachezaji wa Yanga kwa ajili ya msimu wa 2020/21 , imemuwekea dau la milioni 50 ili kumnasa beki wa pembeni wa Nkana Rangers ya Zambia, Hassan Kessy.

Beki huyo ni kati ya wachezaji wanaowaniwa na Yanga katika kuiimarisha safu ya ulinzi ya kulia pamoja na beki wa KMC, Kelvin Kijiri ambaye klabu yake inahitaji Sh 60Mil ili imuachie kutokana na kubakisha mwaka mmoja katika mkataba wake.

Yanga hivi sasa ipo kwenye mipango ya kukisuka kikosi chao baada ya kutangaza kuachana na wachezaji wake 14 wakiwemo mastaa Papy Tshishimbi, David Molinga, Mrisho Ngassa na Issa Mohammed ‘Banka’.

Taarifa zinaeleza kuwa uongozi wa Yanga kwa kushirikiana na GSM walimuita beki huyo Jumapili usiku na kukaa naye mezani kwa ajili ya kufanya mazungumzo ambayo yalishindwa kufikia sehemu mzuri kutokana na dau kubwa ambalo amelitaka

Mtoa taarifa huyo alisema kuwa beki huyo ametaka kitita cha Sh 60Mil kabla ya kupunguza kufikia Sh 55Mil kabla ya viongozi hao kumuwekea dau hilo la 50Mil pekee.

Aliongeza kuwa mabosi hao wamefikia makubaliano ya kumpa Sh 50Mil na mshahara wa Sh 4Mil, ambao nao ameukataa akitaka Sh 6Mil ya mshahara ili asaini.

Bado muafaka mzuri haujafikia kati ya uongozi wa Yanga na Kessy aliyekuwepo kwenye mipango mizuri ya kurejea tena Jangwani baada ya mkataba wake Nkana kumalizika.

“Kikubwa walichoshindwana ni dau la usajili na mshahara pekee lakini mambo mengine kila kitu kinakwenda vizuri, upo uwezekano mkubwa wa beki na uongozi kumalizana ndani ya wiki hii," alisema mtoa taarifa.

Alipotafutwa Kessy kuzungumzia hilo alisema kuwa “Nipo kwenye mazungumzo mazuri na Yanga kama mambo yakienda vizuri nitasaini mkataba, nisingependa kuweka wazi dau la usajili ambalo mimi nilitaka kwani hiyo ni siri yangu na klabu.”

Post a Comment

0 Comments