BETI NASI UTAJIRIKE

KOCHA MPYA WA BARCELONA AMPA MKONO WA KWAHERI SUAREZ


Kocha mpya wa Barcelona amemwambia Luis Suarez atafute timu nyingine kuelekea msimu wa 2020/21.Ronald Koeman hajafurahishwa na uwezo wa mchezaji huyo aliyewahi kuzichezea Ajax na Liverpool.

Suarez anaumri wa miaka 33 na msimu uliomalizika alifanikiwa kufunga mabao 21 kwenye michezo 29 aliyocheza kwenye msimu huo.Tangu ku8wasili Barcelona amecheza michezo 283 akifunga mabao 198. Mchezaji huyo amefanikiwa kuwa mfungaji bora wa La Liga kwa msimu wa 2-17/18 huku akiisaidia timu hiyo kutwaa makombe ya La Liga,Copa Del Rey na UEFA champions league 

Mchezaji huyo anatamani kuendelea kubaki ndani ya Barcelona lakini uongozi wa klabu hiyo unataka kumtumia kama chambo ili kumnasa Van de beek wa Ajax.kama mchezaji huyo ataondoka Barcelona basi bao lake la mwisho ndani ya klabu hiyo ni lile alilofunga dhidi ya Barcelona kwenye mchezo wa nusu fainali dhidi ya Bayern Munich uliomalizika kwa Barcelona kufungwa mabao 8-2

Post a Comment

0 Comments