BETI NASI UTAJIRIKE

KMC WAENDELEA KUJENGA UKUTA WA BERLIN KUELEKEA MSIMU WA 2020-21


Klabu ya KMC imeendelea kujiimarisha kuelekea msimu wa 2020-21 baada ya kumnasa aliyekuwa beki wa kati wa Lipuli David Mwasa. Beki huyo alikuwa ni nguzo muhimu kwa Lipuli hasa msimu uliomalizika 

Nyota huyo amelamba mkataba mnono wa kuichezea timu hiyo kwa miaka miwili.Uongozi wa KMC umeendelea kuimarisha eneo la ulinzi baada ya juzi kumsajili aliyekuwa beki wa Yanga Vicente Chikupe maarufu kwa jina la Dante na sasa wameongeza nguvu kwa kumsajili Mwasa.

Ukuta wa KMC unategemewa kuwa imara kwani mabeki hao wote wawili ni imara sana na hii itaongeza changamoto kwenye ligi

Post a Comment

0 Comments