BETI NASI UTAJIRIKE

KILICHOMPONZA PAPY TSHISHIMBI MPAKA KUACHWA CHAELEZWA


 Uongozi wa klabu ya Yanga umesema kuwa sababu kubwa ya kuachana na nyota wao Papy Tshishimbi ambaye ni nahodha wa kikosi hicho ni kushindwa kufikiana makubaliano kwa pande zote mbili.

Tshishimbi mkataba wake unamalizika rasmi Agosti 12 kwa mujibu wa kaimu katibu, Simon Patrick ambapo atakuwa huru kusepa ndani ya kikosi hicho baada ya jana, Agosti kuwa miongoni mwa nyota walioachwa.

Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa wameachana na Tshishimbi kwa kushindwana pande zote mbili kuelewana.

"Haukuwa ni mpango wote kuachana naye jumla lakini kilichotokea ni kwamba wote tumeshindwa kuelewana hasa kwa upande wa makubaliano.

"Sisi tunachokifanya ni kusikiliza namna mchezaji anavyosema nasi pia tunaweka masharti yetu pale ambapo inashindikana inasababisha tunaachana na mchezaji," amesema Bumbuli.

Post a Comment

0 Comments