BETI NASI UTAJIRIKE

KAULI TATA YA MOHAMMED DEWJI KUHUSU USAJILI YAIBUA MJADALA


Kama wewe ni shabiki wa klabu ya Simba na ulitegemea kuona nyota mbalimbali wanaondolewa na kusajiliwa wengine  kikosini hapo hasa  kipindi hichi cha dirisha kubwa la usajili basi hilo jambo unapaswa kulisahau kwa sasa 

Mwenyekiti wa bodi ya uwekezaji Simba Bw.Mohammed Dewji amesema anaimani na wachezaji waliopo na hana mpango wa kusajili wachezaji wengine . Hii si mara ya kwanza kwa Dewji kutoa kauli hiyo kwani kuna kipindi alisema hata mtoa mchezaji yeyote ndani ya  Simba mara baada ya msimu wa ligi kumalizika 

Leo hii Agosti 04 kupitia mtandao wa Twitter Dewji aliandika "Timu nzuri hazihitaji kusajili sana " Klabu  ya Simba mpaka sasa imemsajili mchezaji mmoja tu ambaye ni straika Charles Illanfya aliyekuwa anakipiga KMC .

Baadhi ya mashabiki wa Simba huko Twitter wameonekana kutokubaliana na kauli ya mwekezaji huyo wakisema eneo la ulinzi la Simba si imara hasa kwenye mechi za kimataifa na wengi wamesema endapo Simba itatolewa mapema basi asitafutwe mchawi.

Je tutegemee kuona Simba wanasajili mchezaji mwingine zaidi ? ama kauli ya Mo Dewji inaashiria watasajili wachezaji wachache zaidi kulinganisha na wapinzani wao Yanga waliosajili mpaka sasa wachezaji wanne, Azam wachezaji wanne.

Post a Comment

0 Comments