BETI NASI UTAJIRIKE

KAPOMBE AFUNGUKA UJIO WA MRITHI HARUNA SHAMTE


Beki bora kabisa mahiri wa kupanda na kushuka upande wa kulia, Shomari Kapombe, amemkaribisha mlinzi David Kameta ambaye amesajiliwa akichukua nafasi ya Haruna Shamte
Kapombe ameeleza kufurahishwa na ujio wa beki huyo kinda, akiamini kuwa ujio wake Simba utaongeza kitu
Aidha Kapombe amesema, Kameta yeye na wachezaji wengine wote wa Simba lengo lao ni moja, kuisaidia Simba iweze kutimiza malengo yake
"Namkaribisha vizuri David Kameta, namtaka aje tufanye kazi kwa ajili ya kuisaidia Simba. Mimi nina uzoefu mkubwa nimecheza miaka 10 kwenye ligi, hatushindani ila tupo hapa kuisaidia timu," alisema Kapombe
Aidha akizungumzia malengo yake ya msimu mpya, Kapombe amesema hatakuwa na maneno mengi lakini kazi yake itaonekana uwanjani
"Pamoja na kuwa nilifanya vizuri msimu uliopita, lakini nahisi kuna kitu kilikosekana, kitu hicho watakiona msimu huu. Sitakuwa na maneno mengi lakini kazi yangu itaonekana uwanjani"

Post a Comment

0 Comments