Inawezekana Yanga wameshindwa kutekeleza masharti ya Papy Tshishimbi ,inasemekana ili mchezaji huyo aongeze mkataba alihitaji apewe gari aina ya Subaru Impreza na hiyo ni moja wapo ya sababu zilizofanya kiungo huyo kutosaini dili jipya la miaka miwili mpaka sasa.
Mkongomani huyo inaelezwa juzi alirudisha kiasi hicho cha fedha alichotanguliziwa ili asaini mkataba wa kuendelea kuichezea timu hiyo katika msimu ujao.
Kiungo huo hivi karibuni alitajwa kuwepo kwenye mazungumzo na uongozi wa Simba kwa ajili ya kukamilisha dili hilo la usajili la kuichezea timu hiyo kwa ajili ya kuiongezea nguvu safu ya kiungo.
Kwa mujibu wa taarifa ambazo zipo ndani ya uongozi wa Yanga, kiungo huyo alikubali kuongeza mkataba wa miaka miwili Yanga kwa dau la Sh 60 pamoja na mshahara wa Sh 10 Mil kwa kila mwezi kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Mtoa taarifa huyo alisema kuwa viongozi hao walikubaliana na kiungo huyo, lakini akabadilika na kuongeza dau la usajili, kufikia Sh 80 Mil ambazo walikataa kuongezea na kufikia makubaliano ya kuachana naye.
Aliongeza kuwa kingine kilichoongeza ugumu ni kiungo huyo kuongeza kipengele cha kupewa gari aina ya Subaru katika mkataba wake, kitu ambacho hakikuwepo katika makubaliano ya awali.
“Tshishimbi inavyoonekana ana sehemu anataka kwenda ndiyo sababu ya kukataa kugomea mkataba tuliompa tangu mwezi Machi, mwaka huu ausaini lakini amekuwa akifanya hivyo.
“Kikubwa anataka kupewa fedha nyingi ya usajili ambayo yeye ameiongeza baada ya makubaliano ya awali kufikia muafaka na kukubali kuongeza mkataba wa miaka miwili kwa dau la Sh 60Mil, lakini baadaye akakataa na kuomba apewe Sh 80Mil.
“Tofauti na dau hilo kuongeza, alitaka mkataba wake uboreshwe kwa kuomba apewe gari aina ya Subaru la kutembelea ambalo kama uongozi tumeona tuachane naye,” alisema mtoa taarifa huyo.
Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Simon Patrick, juzi alisema kuwa: “Hivi sasa tunataka wachezaji wote kuwaweka levo moja, hatutaki kumfanya mchezaji mmoja kuwa spesho katika timu, uongozi hatutakuwa na muda wa kumbembeleza mchezaji katika kipindi hichi ambacho tunajenga timu bora itakayoleta ushindani katika msimu."
0 Comments