BETI NASI UTAJIRIKE

KADUGUDA AFAFANUA SUALA LA USAJILI NDANI YA SIMBA


Kaimu mwenyekiti wa Simba Mwina Kaduguda amewatoa hofu mashabiki wa klabu ya Simba kuelekea msimu wa 2020/21 hasa usajili wa timu hiyo. Kaduguda ameifafanua kauli iliyotolewa na Mwenyekiti wa bodi ya uwekezaji Simba Bw.Mo Dewji aliyeandika kuwa "Timu nzuri hazihitaji usajili.

Kupitia kituo cha redio Kaduguda amenukuliwa akisema " Tunajiandaa kusajili wachezaji wa nne au watano, timu inamapungufu baadhi ya maeneo lakini hatuendi kusajili upya timu yetu kwani kikoi tulichonacho kinajitosheleza. Kaduguda aliongeza  

"Mipango yetu ni kuwa timu kubwa Africa na sio timu kongwe. Kwa hapa nchini timu kongwe ni mbili tu Simba na Yanga lakini sisi hatutaki kuwa timu Kongwe bali timu kubwa itakayofanya makubwa kimataifa. Leo hii ukikaa na watu wa Yanga wanakwambia tuna makombe 27 ya ligi ila ukiwauliza mipango yao ni ipi baada ya kuwa mabingwa wa kihistoria watabaki wanasema wao ni wakongwe 

Simba imekwisha msajili Mshambuliaji kutoka KMC Illanfya na sasa wapo hatua za mwisho kumnasa beki wa Costal Union Ibrahim Awe .Ni wakati wa mashabiki kuwa watulivu kuelekea usajili huo uliokwisha Agosti 1

Post a Comment

0 Comments