advertise with us

ADVERTISE HERE

JUVENTUS IMEFUATA NJIA WALIZOPITA MAN U,CHELSEA,REAL MADRID NA ARSENAL


Mfumo wa kutumia wachezaji wa zamani kama makocha wa timu husika haujaanza jana  wala leo  ila kwa sasa imekuwa dili kubwa kwa vilabu duniani kote. Manchester United walimkabithi nafasi ya ukocha  OleGunnar mchezaji aliyewapa makombe mengi Manchester United miaka ya 90. Chelsea wamemkabidhi timu frank Lampard kuinoa na ikumbukwe mchezaji huyo wa zamani aliitumia asilimia 90 ya maisha yake ya soka kuitumikia Chelsea. 

Mikel Arteta aliwahi kuichezea timu ya Arsenal enzi za Arsene Wenger na sasa anainoa timu hiyo huku akiwa na historia ya kuiongoza timu  hiyo kutwaa ubingwa wa FA. Zinedine Zidane amekua akiifundisha Real Madrid kwa miaka mitano sasa huku akiipa timu hiyo ubingwa wa ulaya mara tatu mfululizo. Ikumbukwe Zidane aliituumikia vyema Real Madrid kama mchezaji na kuwapa makombe mbalimbali.



Klabu ya Juventus imemfuta kazi kocha wake Mario Sarri na kumkabidhi aliyekuwa mchezaji wao wa zamani Andrea Pirlo.Juve wamefanya maamuzi ya kumfuta sarri baada ya kuondolewa ligi ya mabingwa hatua ya 16 bora tena na timu kama Lyon.

Andrea Pirlo alikuwa mchezaji wa Juventus kuanzia mwaka 2011 hadi 2015 akicheza michezo 119 na kufunga mabao 16. Swali linakuja kuuliizwa ni je Pirlo anastahili kutwaa nafasi ya Sarri? 

Post a Comment

0 Comments