BETI NASI UTAJIRIKE

MESSI NA RONALDO ENZI ZAO ZIMEKWISHA PITA


Ni kama enzi za Ronaldo na Messi zimekwisha pita kwani kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2006 wachezaji Lionel Messi na Cristiano Ronaldo wamekosekana kwenye kikosi bora cha  ligi ya mabingwa ulaya msimu wa 2019/20. Bayern Munich mabingwa wa kombe hilo ndiyo waliotawala kikosi hicho.

Kikosi hicho cha wachezaji 11 kimewataja nyota nyota 10 kutoka Bundesliga huku 8 kati yao wakitoka Bayern Munich ,mmoja kutoka Borrusia Dortmund na mwingine kutoka RB.Leipzig huku mmoja akitoka Ligue 1 ya Ufaransa PSG

Robert Lewandoski mwenye mabao 15 ndiye aliyetwaa kiatu cha mfungaji bora na amejumuishwa na Haaland mwenye mabao 10 kama washambuliaji, Neymar ametajwa kama winga wa kushoto huku Gnarbry akiwa winga wa kulia . Thomas Muller na Thiago Alcantara ni viungo huku Davies beki wa kushoto ,Joshua Kimmich akiwa beki wa kulia,Dayout Upamecano wa RB Leipzig na David Alaba wakiwa mabeki wa kati huku Manuer Neuer akiwa golikipa wa timu hiyo.

Post a Comment

0 Comments