BETI NASI UTAJIRIKE

JE KOCHA HUYU ATAFAA KURITHI NAFASI YA EYMAEL NDANI YANGA


Kocha Mkuu wa Kagera Sugar Mecky Mexime amesema kuwa yupo tayari kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na  Luc Eymael ambaye amefutwa kazi na klabu ya Yanga. Mexime amekuwa akitamani kuifundisha Yanga Tangu mwanzni mwa msimu wa 2019/20 huku pia akitaka kuchukua nafasi ya Mwinyi Zahera alipotimuliwa kisha Eymael akakabidhiwa timu . Mexime amesema ikiwa mazungumzo yatakwenda sawa basi atajiunga na mabingwa wa kihistoria
Eymael, raia wa Ubelgiji alifutwa kazi na uongozi wa Yanga, Julai 27 baada ya kuongea maneno yaliyokuwa yakiashiria ubaguzi wa rangi kwa mashabiki pamoja na kusema kuwa hafurahishwi na mashabiki wa hapa kwa kuwa hajui soka.
Maxime ambaye amekuwa bora ndani ya   kikosi cha Kagera Sugar kwa msimu wa 2019/20 baada ya kumaliza kikiwa nafasi ya nane na pointi 52 alinukuliwa akisema kuwa yupo tayari kufanya kazi ndani ya Yanga.
Mimi nipo Kagera Sugar kwa sasa ndipo ambapo ninafundisha, ikitokea Yanga wakahitaji kupata huduma yangu ni suala la mazungumzo, sina tatizo ikiwa kila kitu kitakuwa sawa nitafanya kazi pale, timu yoyote ile ambayo inahitaji huduma yangu ninaweza kufanya nao kazi,” alisema Maxime.

Post a Comment

0 Comments