BETI NASI UTAJIRIKE

HIKI HAPA CHUMA KIPYA CHA NAMUNGO FC


Klabu ya Namungo FC imeanza kujiandaa na michuano ya kimataifa kwa kusajiliwahezaji wa viwango vya juu,Klab hiyo imemsajili kiungo aliyekuwa anaichezea Lipuli Fredy Tangalo. kiungo kiungo huyo amesaini miaka miwili ndani ya Klabu ya Namungo FC ya Lindi.

Kiungo huyo amesaini dili hilo akiwa ni mchezaji huru baada ya mkataba wake kuisha ndani ya Klabu ya Lipuli huku timu hiyo ikishuka daraja.
Tangalo anakuwa ni mchezaji wa kwaanza kusajiliwa na Namungo kwa matumizi ya msimu wa 2020/21

Namungo inaimarisha kikosi chake kwa sasa kwa ajili ya msimu ujao ambapo ina nafasi ya kushiriki mashindano ya Kimataifa itapeperusha Bendera ya Taifa ya Tanzania kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho. 

Nafasi hiyo wamepata baada ya kutinga fainali ya Kombe la Shirikisho na kukutana na bingwa wa ligi Simba ambaye alishinda kwa mabao 2-1 Uwanja wa Nelson Mandela, licha ya kupoteza imepata nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa kwa kuwa tayari Simba itaiwakilisha nchi Kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

Post a Comment

0 Comments