BETI NASI UTAJIRIKE

NI HABARI NJEMA KWA AU MBAYA KWA MASHABIKI WA YANGA?


Papy Tshishimbi, amekubali kuongeza mkataba wa kuendelea kuitumikia Yanga.Hiyo ikiwa ni siku chache tangu uongozi wa timu hiyo utangaze kuachana naye pamoja na wengine ambao mikataba yao imemalizika.

Taarifa ambazo imezipata Spoti Xtra, kutoka kwa rafiki wa karibu wa Tshishimbi, nyota huyo mwenyewe amewafuata viongozi wa Yanga na kuomba asaini mkataba wa mwaka mmoja kwa dau la Sh Mil 60 badala ya Sh Mil 80 alizowekewa awali na waajiri wake.

Mtoa taarifa huyo alisema kiungo huyo ameyaondoa baadhi ya mahitaji yake aliyoyaomba kwenye mkataba wake mpya aliopewa ikiwemo gari.

Aliongeza kuwa baada ya kiungo huyo kurudi kwa viongozi, aliwekwa pembeni na kuambiwa ataitwa kwa ajili ya mazungumzo mapya kabla ya kupewa mkataba huo mpya.

Tshishimbi amekubali yaishe na kuomba kusaini mkataba mpya wa kuendelea kubaki Yanga ni baada ya yeye mwenyewe kuwafuata viongozi na kuomba kupunguza dau la usajili na mahitaji yake ya gari aliloliomba.

“Ukweli ni kwamba amepunguza dau la usajili alilokuwa analitaka awali ambalo ni Sh Mil 80 na mshahara wa Sh Mil 10. Sasa anataka Sh Mil 60 za usajili.

"Haya yote ameyafanya baada ya kuona yupo kwenye orodha ya majina ya wanaoachwa. Alivyorudi kwa viongozi wakamwambia asubiri ataitwa kwa ajili ya majadiliano mapya,” alisema mtoa taarifa huyo.

Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, wakili Simon Patrick, hivi karibuni alisema: “Tumeshindwa kufikia muafaka mzuri na Tshishimbi na kuamua kuachana naye, kikubwa tulitaka kuwaweka wachezaji wote katika levo na siyo kumfanya mmoja mkubwa kabla ya kuchukua uamuzi huo."

Post a Comment

0 Comments