Tetesi ni kuwa Bernard Morrison ameshamalizana na uongozi wa Simba hivyo anaweza kutangazwa muda wwote kuanzia leo Agosti 7.Habari zinaeleza kuwa Morrison tayari ameshamalizana na Simba kilichobaki kwa sasa ni kutangazwa ndani ya kikosi hicho cha Simba.
'Tayari Simba wamemalizana na Morriosn kilichobaki ni kutangazwa tu ndani ya kikosi hicho," ilieleza taarifa hiyo.
Hersi Said ambaye ni Mkurugenzi wa Uwekezaji ndani ya GSM ambao ni wadhamini wa Yanga amesema:"Inashangaza kwa kuwa bado Morrison ana mkataba na kesi yake bado inaskilizwa, hivyo itakuwa ni ajabu kutangazwa leo najua kamati inafuatilia mambo yaliyopo
"Kwa harakaharaka nimegundua kwamba mchezaji ni wetu, nikiangalia naona picha mbaya sana kama mchezaji atasaini na amekuwa na matatizo ya nidhamu kwa muda mrefu, amekuwa akisema kwamba viongozi wa Simba wamekuwa wakimlaghai ili kumpa mkataba hivyo kama atatangazwa leo basi itatoa picha kwamba Simba walikuwa nyuma katika haya," amesema.
0 Comments