BETI NASI UTAJIRIKE

DIAMOND KUACHIA WIMBO KUIPONGEZA SIMBA KWA UBINGWA


Msemaji wa klabu ya Simba Haji manara ametangaza rasmi kwamba Diamond Platinumz ni mmoja ya wageni waalikwa watakaopanda jukwaani kutumbuiza kwenye siku ya Simba Day. Manara amesema wasanii watakaotumbuiza siku hiyo ni Meja Kunta,Diamond Platinumz, Tundaman [amoja na bendi ya mziki Twanga pepeta.

Manara alisema Simba Day burudani itatolewa na Twanga Pepeta, Tunda Man, Meja Kunta, Mwasiti na kipekee atakuwepo Diamond Platinumz. Litakuwa kama tamasha la mziki, amekusudia kufanya jambo kubwa na kwa kupitia hilo kesho alhamisi kutakuwa na BIG SURPRISE kwa Wanasimba. MC atakuwa Mpoki."

Itakumbukwa Diamond aliahidi kwa klabu ya Simba kwamba endapo itatwaa makombe mawili msimu wa 2020-21 basi atatoa zawadi ya nyimbo ihusuyo Simba .Mashabiki wa Simba wajiandae ngoma mpya kutoka kwa msanii huyo.

Post a Comment

0 Comments