BETI NASI UTAJIRIKE

CRISTIANO RONALDO ASHINDWA KUIOKOA JUVENTUS DHIDI YA LYON


Klabu yaJuventus imeaga rasmi michuano ya ligi ya mabingwa ulaya kwa msimu wa 2019/20. Juventus wametolewa kwa goli la ugenini baada ya mchezo wa kwanza kufungwa bao 1-0 dhidi ya Lyon na mchezo wa pili uliochezwa hapo jana na Juventus kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 na kufanya timu hizo kufungna mabao 2-2 lakini Lyon alikuwa na faida ya bao 1 baada ya kufungwa ugenini mabao 2-1.

Memphis Depay alikuwa wa kwanza kuwapa Juventus bao la kuongoza dakika ya 12 kwa mkwaju wa penati lakini Cristiano alisawazisha bao hilo dakika ya 43 kisha kufunga bao la pili dakika ya 60 ya mchezo huo mabao ambayo hayakutosha kuivusha Juventus.

Lyon wamefanikiwa kuingia robo fainali za ligi ya mabingwa ulaya kwa msimu wa 2019/20 huku Juventus wakiondoshwa moja kwa moja kwenye michuano hiyo.

Post a Comment

0 Comments