BETI NASI UTAJIRIKE

CORONA YAVAMIA KAMBI YA ATLETICO MADRID KUELEKEA MCHEZO DHIDI YA RB.LEIPZIGKlabu ya Atletico Madrid imekiri kuwa wachezaji wake wawili wamekumbwa na virusi vya corona.Alhamis hii Atletico watakuwa na mchezo wa Uefa robo fainali dhidi ya RB.Leipzig mchezo utakaopigwa jijini Lisbon nchini Ureno.

Taarifa ya klabu hiyo ilisema wachezaji na viongozi waliotakiwa kwenda Lisbon kwa mchezo huo walifanyiwa vipimo na wawili kati yao walikutwa na maambukizi hivyo kulazimika kujitenga kwa kubaki majumbani mwao.

Wachezaji waliokutwa na Corona ni Mshambuliaji raia wa Argentina Angel Correa na beki wa pembeni raia wa Crotia Sime Vlsaljko na wachezaji hao wamelazimika kujitenga majumbani mwao.

Kupatikana kwa waathirika wa Corona ndani ya kikosi cha Atletico kunaweza kusababisha kikao cha dharula kuhusiana mechi ya Altetico Madrid dhidi ya RB. Leipzig  na kama mambo yatakwenda ndivyo sivyo basi hatma ya michuano hiyo itawekwa wazi.

Ikumbukwe Hispania inongoza kwa kuwa na maambukizi kwa bara la ulaya kwa kufikisha wagonjwa 314,000 huku zaidi ya watu 28,000 wakipoteza maisha 

Post a Comment

0 Comments