BETI NASI UTAJIRIKE

CLATOUS CHAMA NA UUNGWANA WAKE NDANI NA NJE YA UWANJA


Baada ya kuisaidia klabu yake ya Simba kutwaa mataji matatu msimu wa 2019/20 Kiungo Clatous Chama alitwaa tuzo ya mchezaji bora wa timu hiyo na kukabidhiwa kiasi cha shilingi milioni 1 na wadhamini wa klabu hiyo kampuni ya Sport Pesa. 

Chama aliahidi fedha hiyo itatumika kuwasaidia watoto wanaoishi mazingira magumu na ameikamilisha ahadi hiyo kwa kupeleka kiasi cha shilingi milioni 1 alichozawadiwa kwa watoto Yatima waishio kituo cha Maunga Kinondoni jijini Dar es Salaam

Chama anasifa za kiungwana kuanzia ndani ya uwanja ambao amekuwa akiwasaidia washambuliaji wa timu hiyo kupata mabao rahisi huku yeye akitengeneza nafasi adhimu sana.

Hizi ni baadhi ya picha za Chama akikabidhi msaada huo
Post a Comment

0 Comments