ads

adds

CHUMA CHA TANO CHASAJILIWA AZAM FC,CHAANZA NA MBWEMBWE


Klabu ya Azam imefanikiwa kumnasa David Mapigano Kisu aliyekuwa kipa namba moja wa Gor Mahia,mwenye rekodi ya kufunga bao la umbali mrefu akifunga moja kwa moja kutoka golini kwake mpaka golini kwa Bandari fc mchezo uliomaliza kwa Gormahia kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 . Azam walimtangaza mchezaji huyo kupitia mitandao ya kijamii na walisema 
Azam FC tunayofuraha kuwataarifu kuwa, tumekamilidha usajili wa golikipa wa kimataifa wa Tanzania, David Mapigano Kissu, kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Gor Mahia ya Kenya.
Kissu ambaye yumo kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars', usajili wake ni sehemu ya mapendekezo ya benchi la ufundi la Azam FC.
Kipa huyo aliyechezea timu za Njombe Mji na Singida United, kabla ya kutimkia nchini Kenya, amekuwa na msimu nzuri akiwa na Gor Mahia, takwimu zikionyesha amecheza jumla ya mechi 15, huku akiwa hajaruhusu wavu wake kuguswa (clean sheet) katika mechi tisa kati ya hizo.
Nyota huyo aliyekuwa kipa namba moja wa Gor Mahia, pia aliweka rekodi ya kufunga bao, akifunga kwa mpira mrefu wa moja kwa moja, wakati Gor Mahia ikiilaza Bandari mabao 3-0.
Huo ni usajili wa tano kwenye kikosi cha Azam FC kwa ajili ya msimu ujao, wengine waliosajiliwa wakiwa ni Awesu Awesu, Ally Niyonzima, Ayoub Lyanga na Ismail Aziz Kada.

Mara baada ya kusajiliwa tu kipa huyo alijiunga n timu hiyo kwenye mazoezi huku akionyesha umahili mkubwa.

Post a Comment

0 Comments