BETI NASI UTAJIRIKE

CHELSEA YAONDOLEWA KWA AIBU KUBWA UEFA


Klabu ya Chelsea imekubali kipigo cha mabao 4-1 kutoka kwa Bayern Munich .Mchezo wa pili wa 16 huo ulipigwa dimba la Alianz Arena, kwa matokeo hayo Bayern Munich imetinga hatua ya robo fainali ligi ya mabingwa ulaya baada ya kufunga jumla ya mabao 7-1 dhidi ya Chelsea kwenye michezo miwili waliyokutana hatua ya hiyo ya 16 bora. 

Robert Lewandowski alikuwa wa kwanza kupachika bao la kwanza kwa mkwaju wa penati dakika ya 10,Ivan perisic akifunga bao la pili dakika ya 24 na Tammy Abraham kutoka Chelsea alifunga bao la kufutia machozi dakika ya 44.Mchezo ulikwenda mapumziko huku Bayern Munich wakiwa mbele kwa mabao 2-1.

Corentin Tolliso aliipa Bayern Munich bao la tatu dakika ya 76 huku Lewandowski akishindilia bao la nne dakika ya 83.Bayern Munich inaungana na klabu za Manchester City ,Lyon ,Barcelona ,psg,Atlanta,Atletico Madrid na RB Leipzig.Post a Comment

0 Comments