BETI NASI UTAJIRIKE

CHELSEA YACHINJWA WEMBLEY ARSENAL WAKIWEKA REKODI MPYA FA


Klabu ya Arsenal imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 mchezo wa fainaliya FA  dhidi ya chelsea. Mchezo huo uliokuwa mkali ulimfanya Piere Aubemayang azidi kulipaisha bara la Africa baada ya kufunga mabao mawili murua .

Chelsea walikuwa wa kwanza kupata bao la kuongoza kupitia Christian Pulisic dakika ya 5 ya mchezo huo lakini bao hilo halikudumu baada ya Piere Aubemayang kusawazisha dakika ya 28kwa mkwaju wa penati baada ya kuchezewa rafu na beki wa Chelsea Azipilicueta.

Mchezo ulikwenda mapumziko kwa timu hizo kuwa sare ya mabao 1-1. Aubemayang alirejea tena nyavuni mwa chelsea dakika ya 67 kwa kufunga bao murua kabisa lililoifanya Arsenal kutwaa kombe la FA msimu wa 2019/20

Ushindi wa fainali hiyo unaifanya Arsenal kuwa klabu  yenye makombe mengi zaidi ya FA ikiwa na makombe 13 tangu kuanzisha kwa michuano hiyo. 

Kikosi cha Arsenal kilikuwa na D.Martinez,Holdings ,David Luiz,Tierney,Bellerin,Cellabos,Xhaka,Maitland-Niles,N.Pepe,Aubemayang  na Lacazzete 

Chelsea walianza na Caballero,Azipilicueta ,Zouma,Rudiger,James ,Joginho,Kovavic,Alonso ,Mount,Giroud na Pulisic

Post a Comment

0 Comments