BETI NASI UTAJIRIKE

KIKOSI CHA SIMBA CHAMCHANGANYA SVEN


Kocha Mkuu wa Simba, mabingwa wa nchi Sven Vandenbroeck amesema ndani ya siku tano anapaswa kupata kikosi chake cha kwanza tayari kwa msimu mpya wa ligi kuu ya Vodacom
Simba inaendelea na kujifua kwenye uwanja wake wa Mo Simba Arena wakijiandaa na mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Namungo Fc ambao utapigwa Jumapili August 30
Sven ameeleza kuridhishwa na kiwango kinachoonyeshwa na wachezaji wote 29 lakini analazimika kuchangua kikosi cha wachezji 18 tu wa kuwatumia katika mchezo mmoja

"Nina wachezaji 29 wanaotakiwa kucheza ni 11 na wengine saba wa kukaa benchi, inaweza ikatokea mchezaji akakosekana kabisa kwenye kikosi cha wachezaji 18"
"Wachezaji wanapaswa kulielewa hili, wasikasirike kwani ukweli nitakuwa na wakati mgumu katika kuchagua"
"Mpaka sasa nina siku tano na kila mmoja anaonyesha anataka kucheza, ila ngoja tuone ingawa najua wapo ambao hawatafurahia kukaa nje," alisema Sven

Post a Comment

0 Comments