BETI NASI UTAJIRIKE

BAADA YA SARPONG MASHINE MPYA INATUA HIVI KARIBUNI


Klabu ya Yanga imefanikiwa kumkaribisha nchini mshambuliaji wa Ghana Michael Sarpong. Mashabiki wa klabu hiyo kama kawaida yao walifika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere kumpokea mshambuliaji mpya wa timu hiyo Michael Sarpong

Sarpong alipokelewa na Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM, Mhandisi Heri Said ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya MashindanoUjio wake unafunga hesabu kwenye safu ya ushambuliaji kwani katika nafasi hiyo ataungana na Mburkinabe Yacouba Soghne na wazawa Waziri Jr na Ditram Nchimbi

Sasa wanasubiriwa wachezaji wawili Yacouba na Carinhos Carmo 'KDB', Kiungo mshambuliaji ambaye anasubiri majibu yake ya corona kabla ya kuruhusiwa kusafiri kutoka AngolaNyota hao wanatarajiwa kuwasili wikiendi hii

Post a Comment

0 Comments