BETI NASI UTAJIRIKE

DEWJI AMZAWADIA JEZI MAALUM SHABIKI WA TIMU HIYO DIAMOND


Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi klabu ya Simba Bilionea Mohammed Dewji 'Mo' amemkabidhi jezi Msanii na Mkurugenzi wa Wasafi Media Nasib Abdul maarufu Diamond Platinumz
Mapema leo, Mo akiongozana na Msemaji wa Simba Haji Manara, walifanya mahojiano maalum redio Wasafi kuelekea tukio kubwa la kilele cha wiki ya Mabingwa, Simba Day litakalofanyika keshokutwa Jumamosi katika viwanja vya Mkapa na Uhuru
Akiwa mdau mkubwa wa Simba, Diamond ametunga wimbo maalum wa hamasa ambao atautumbuiza siku ya Jumamosi
Diamond atapewa takribani saa zima kuwapa burudani mashabiki wa Simba wanaotarajiwa kujitokeza kwa wingi katika tukio hilo la aina yake
Wimbo maalum ulioandaliwa na Diamond, ulitambulishwa leo Wasafi FM

Post a Comment

0 Comments