BETI NASI UTAJIRIKE

BAYERN MUNICH YATWAA KOMBE LA TATU MSIMU WA 2019/20


Klabu ya Bayern Munich imefanikiwa kutwaa taji lake la sita la UEFA baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya PSG. Shukrani za kipekee zimwendee winga Coman aliyefunga bao zuri kwa kichwa.

Hili linakuwa ni kombe la 6 kwa klabu hiyo tangu kuanza kushiriki michuano hiyo. Msimu wa 2019-20 Bayern Munich hajapoteza mchezo wowote kwenye michuano ya UEFA huku ikiwa imefunga jumla ya mabao 41 kwenye mechi 11 walizocheza.

Robert Lewandowski ameibuka kinara wa ufungaji kwenye michuano hiyo kwa kufunga mabao 15 kwenye mechi 10 alizocheza huku pia akiwa ni mchezaji aliyetengeneza mabao mengi akifanya hivyo mara 6.

Hili linakuwa kombe la tatu kwa klabu hiyo kushinda msimu huu. Imeshinda Bundesliga,Kombe la Ujerumani na sasa ni ligi ya mabingwa ulaya.

Post a Comment

0 Comments