BETI NASI UTAJIRIKE

BAADA YA SAKATA LA MORRISON KUMALIZIKA JINGINE LAIBUKA YANGA


Klabu ya Yanga imejikuta mtegoni baada ya msemaji wa Azam FC Zaka zakazi kudai kwamba klabu hiyo ilitunga barua kuonyesha Mchezaji wake Abubakar Salum anataka kuondoka klabuni hapo na kujiunga na mabingwa wa kihistoria.

Suala hilo liliibua sintofahamu kwa mchezaji Abubakar Salum aliyekana kuandika barua hiyo huku uongozi wa azam ukishusha lawama kwa Yanga. Uongozi wa Yanga kupitia afisa habari wake Hassan Bumbuli ulikana barua hiyo na Bumbuli alisema 

"tumeisikia sauti ya msemaji wa Azam FC akiishutumu Yanga SC, kiukweli ni shutuma nzito sana ambazo kamwe hatuwezi kuzipuuza. . Tunamtaka ajitokeze tena amtaje huyo mtu anayedai ni wa Yanga SC aliyepeleka barua inayomhusu Sureboy kutaka kuhama, wafanyakazi wote wa Yanga wa Id Number na kama kweli ni mfanyakazi Yanga tumjue alikuwa na malengo gani kwa maana kitendo hicho hakiwezi fanywa na uongozi wa Yanga. . kama aliropoka ili kutafuta kiki ama followers aitake radhi Yanga na kukanusha ama sivyo tutaenda mbele zaidi. . kumekuwa na wimbi la watu kuisema Yanga vibaya ili tu wapate umaarufu kama msemaji wa klabu moja, kuisema Yanga ndio kula yake. . sasa tunataka kukomesha hii tabia tutaanza na huyo msemaji wa Azam"

Post a Comment

0 Comments