BETI NASI UTAJIRIKE

ARTETA AWEKA REKODI MPYA ARSENAL IKITWAA FA


Kocha mkuu wa Arsenal ameweka rekodi mpya kwenye michuano ya FA nchini uingereza baada ya kuibuka kidedea kwenye fainali ngumu iliyopigwa dimba la Wembley jijini London. Kwenye mchezo huo mzuri wa kuvutia Arsenal waliibuka na ushindi wa mabao 2-1 na shukrani za pekee zimwendee Piere Aubemayang aliyefunga mabao yote mawili.

Mikel Arteta anakuwa kocha  wa kwanza kutwaa kombe la FA akiwa mchezaji wa klabu ya Arsenal na akiwa kocha wa klabu hiyo. Hakuna kocha yeyote aliyewahi kuweka  rekodi kama hiyo mpaka sasa.

Itakumbukwa kocha huyo alikabidhiwa timu hiyo Disemba 2019 baada ya aliyekuwa kocha wa timu hiyo Unai Emery kushindwa kuiongoza kufanya vizuri kwa  timu hiyo kwa misimu miwili mfululizo.


Post a Comment

0 Comments