BETI NASI UTAJIRIKE

ZIFAHAMU REKODI 7 ALIZOWEKA RAMOS. AWAPOTEZA MESSI,FIGO,ZIDANE,INIESTA


Beki nambari moja Duniani Sergio Ramos ameendelea kuwa nguzo muhimu kwa klabu ya Real Madrid baada ya kuipa ushindi klabu hiyo wa bao 1-0 la mkwaju wa penati dhidi ya Athletic Club. 

Mchezo huo mgumu uliopigwa dimba la San Mam├ęs Stadium huku Ramos akiwa mchezaji bora wa mchezo baada ya kupiga penati maridadi dakika 73 ya mchezo. Ramos  amekuwa mkombozi wa real Madrid huku akifunga mabao 11 msimu huu La Liga 

Tangu kurejea kwa La Liga msimu huu Ramos amefunga jumla ya mabao 5 kwenye mechi 6 alizocheza na kumfanya awe na mabao mengi zaidi ya mchezaji yeyote tangu ligi hiyo iliporejea Juni 12.

Ramos anakuwa mchezaji wa pili nyuma ya Benzema kwa wingi wa mabao akifunga mabao 10 huku Benzema akiwa na mabao 17.

Rekodi za Ramos 

1. Ni  beki mwenye mabao mengi zaidi msimu huu akifunga mabao 12 kwenye michuano yote na 10 La Liga

2.Ramos ndiye beki mwenye mabao mengi zaidi La Liga akifunga mabao 71

3. Anashika nafasi ya pili kwa wingi wa magoli ndani ya La Liga akifunga mabao 12 michuano yote.

4. Anagoli moja la Faulo sawa na Ronaldo msimu huu 

5.Anamagoli 71 La Liga akiwafunika Xavi mabao 58,Iniesta mabao 35,Luis Figo mabao 68 Luis Figo mabao 70 Neymar mabao 68 Zidane mabao 38

6.Amekuwa na mabao 10 mengi zaidi msimu huu kwa kuwazidi Antonio Griezman mabao 9 ,Lacazette mabao 8,Diego Costa mabao 4 ,Roberto Firmino mabao 4

7.Amefunga mabao matano tangu kurejea kutoka Lock Down akiwafunika Lionel Messi mabao 3 na Cristiano Ronaldo mabao 4

Post a Comment

0 Comments