BETI NASI UTAJIRIKE

YANGA WAZUNGUMZIA UWEPO WA MORRISON DHIDI YA SIGIDA UNITED LEO


Klabu ya Yanga imesema kuwa suala la Bernard Morrison kurejea ndani ya timu hiyo na kuwa Kwenye kikosi kitakachowavaa Singida United leo lipo mikononi mwa benchi la ufundi.

Benchi la ufundi la Yanga linaongozwa na Kocha Mkuu, Luc Eymael raia wa Ubelgiji ambaye kwenye mchezo uliopita, Julai 12 wa hatua ya nusu fainali dhidi ya Simba alimchezesha kiungo huyo dakika 64 na nafasi yake ikichukuliwa  na Patrick Sibomana. 

Baada ya kutolewa nje, Morrison aligoma kukaa benchi na kutoka jumla nje ambapo inaelezwa kuwa alipanda bodaboda na kusepa Uwanja wa Taifa jambo lililowakasirisha mashabiki wa Yanga pamoja na viongozi.

Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa suala la Morrison kurejea kikosini na kambini lipo mikononi mwa benchi la ufundi.

"Kuhusu Morrison suala lake la kuwa ndani ya kikosi ama kurejea kambini  lipo mikononi mwa benchi la ufundi wao ndio watatuambia kama wanamhitaji au la kwani ndio kazi yao," amesema.


Mchezo huo Yanga ilikubali kuyeyusha tiketi ya kusonga hatua ya fainali ya Kombe la Shirikisho baada ya kufungwa mabao 4-1.Hii leo Yanga inacheza na Singida United Uwanja wa Uhuru mchezo wa Ligi Kuu Bara.

Post a Comment

0 Comments