Klabu ya Yanga imesema kuwa nahodha wao Papy Tshishimbi yupo fiti kwa ajili ya mchezo dhidi ya Simba utakaochezwa Uwanja wa Taifa hii leo.Mchezo huo hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na kila timu kuhitaji matokeo mazuri. Ofisa Uhamasishaji wa Klabu ya Yanga Antonio Nugaz amesema kuwa kila kitu kuhusu mchezo wa kesho kipo sawa wanasubiri wakati ili watoe burudani kwa mashabiki pamoja na soka safi. "Tupo sawa na tutatoa burudani safi kwa mashabiki na malengo yetu ni kupata ushindi, bila makandomakando hatufungwi sisi, tupo vizuri na mambo yatakuwa uwanjani. "Wachezaji wote wapo sawa kuanzia Tshishimbi yupo vizuri hivyo ni jukumu la mwalimu mwenyewe kujua anaanza na nani ila kikosi na wachezaji wote kiujumla wapo tayari tukutane Taifa kuona namna itakavyokuwa," amesema. Mshindi wa mchezo wa kesho atacheza na Namungo hatua ya fainali ya Kombe la Shirikisho itakayochezwa Sumbawanga. Tshishimbi alikuwa nje ambapo alikosa mechi za hivi karibuni ikiwa ni pamoja na zile mbili walizocheza mkoani kati ya Biashara United ambapo iliisha kwa sare ya bila kufungana pamoja na ile ya Kagera Sugar ambapo Yanga ilishinda bao 1-0 kwa kuwa alikuwa unasumbuliwa na goti. Leo alikuwa miongoni mwa wachezaji waliokuwa wanafanya mazoezi kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo wa kesho.
0 Comments