BETI NASI UTAJIRIKE

YANGA WAONYESHA MABADILIKO KWA VITENDO DKT.MSOLLA AGEUKA SHUJAA KWA HILI


Mwenyekiti wa klabu ya Dkt Mshindo Msollla amekuwa mbunifu kwa mambo mbalimbali ndani na nje ya uwanja. Kitendo cha kuipeleka Yanga kwenye maonyesho makubwa kabisa nchini ya Sabasaba kwa mara ya kwanza linakuwa jambo lenye sura chanya hasa kwa klabu hiyo yenye makao makuu mitaa ya twiga na jangwani.

Yanga wanafanya mabadiliko ya kimfumo na kiuongozi na mabadiliko hayo yanategemewa kuchukua miaka minne kuweza kukamilika. kitendo cha Yanga kupeleka baadhi ya makombe,kuuza jezi na kufanya maonyesho ndani ya viwanja vya  Sabasaba ni dalili tosha wanaleta mabadiliko chanya.

Kama ni mipango ya msolla basi nasema amefanikiwa kuifanya Yanga ionekane timu ya Wananchi kama wao wanavyojiita lakini pia staili waliyotumia itavutia maelfu kuifahamu klabu hiyo kwa undani. 

Sisi kama Amospoti.com tumejiandaa kufanya mahojiano na viongozi mbalimbali wa Yanga watupe maoni ya maono haya ya mwenyekiti msola kuwa karibu nasi.

Post a Comment

0 Comments