BETI NASI UTAJIRIKE

WAGONGA NYUNDO WA LONDON WAIANGAMIZA CHELSEA


Klabu ya Chelsea imeshindwa kutwaa nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi baada ya kukubali kipigo kutoka kwa Westham. Mchezo huo mkali uliopigwa dimba la London Stadium ulikuwa ni vuta nikuvute huku chelsea akikubali kipigo cha mabao 3-2 .

Willian alikuwa wakwanza kufungua nyavu za Westham kwa mkwaju wa penati dakika ya 42 lakini Soucek alisawazisha bao hilo kabla ya kwenda mapumziko. Michail Antonio alifunga bao dakika ya 51 lakini Wilian alirudi nyavuni na kusawazisha bao hilo dakika ya 72. Andriy Yamolenko  alipigilia msumari dakika ya 89 na kuifanya Chelsea kuondoka kwa majonzi uwanjani.

Kwa matokeo hayo Chelsea inabaki nafasi ya 4 ikiwa na pointi 54 kwenye michezo 32 waliyocheza.Huku Westham ikifikisha pointi 30 kwenye michezo 32 waliyocheza na kupanda mpaka nafasi ya 16 kwenye msimamo wa ligi

Post a Comment

0 Comments