BETI NASI UTAJIRIKE

WAFAHAMU WAFUNGAJI TANO BORA KARNE YA 21


Mshambuliaji wa Juvenus na Ureno Cristiano  Ronaldo ndiye anayeongoza kwa kuwa na mabao mengi zaidi kwa wachezaji wa karne ya 21 huku pia akiongoza kwa kucheza mechi nyingi kuliko mshambuliaji yeyote. Nakuletea orodha ya wachezaji wenye mabao mengi zaidi 

5.Luis Suarez 

Mshambuliaji huyu hatari wa Barcelona raia wa Uruguay anashika nafasi hiyo kwa kufunga mabao 477 akicheza michezo 761 na kumfanya kuwa na wastani wa 0.63 kufunga kwenye kil mechi. Suarez anayetumikia Barcelona alianza soka la kulipwa mwaka 2005 klabu ya Nacional akicheza Ajax na Liverpool.

4. Robert Lewandowski

Mfungaji huyu makini wa Bayern Munich amekuwa akiweka rekodi za kipekee kila msimu ndani ya Bundesliga. Kwa sasa amefunga mabao 482 kwenye michezo731 aliyocheza sawa na wastani wa 0.66 Kufunga kila mechi. Alianza soka la kulipwa mwaka 2006 klabu ya Znicz na sasa yupo Bayern Munich 

3. Zlatan Ibrahimovic 

Raia huyu wa Sweden amekuwa moto wa kuotea mbali kila msimu akiwa amefunga mabao 547 kwenye michezo 926 akiwa na wastani wa 0.59 kufunga bao kila mchezo.Zlatan alianza soka mwaka 1999 klabu ya Malmo Sweden huku sasa akiitumikia AC Milan

2.Lionel Messi 

Mshambuliaji huyu ndiye bora muda wote akiwa a mabao 727 kwenye michezo 917 aliyocheza tangu anaanza soka huku akiwa na wastani wa 0.79 kufunga kila mchezo . Messi alianza soka mwaka 2003 klabu ya Barcelona C na mpaka sasa anaitumikia klabu hiyo

1. Cristiano Ronaldo 

Anaongoza orodha hii kwa kuwa mshambuliaji aliyecheza michezo mingi zaidi mechi 1041 akifunga mabao 746 na kumfanya aongoze orodha ya wafungaji huku akiwa na wastani wa 0.72 kufuga kila mechi.Alianza soka maka 2001 klabu ya Sporting CB C na sasa yupo Juventus

Post a Comment

0 Comments