BETI NASI UTAJIRIKE

UONGOZI YANGA WATOA TAMKO RASMI KUFUATIA AJALI

Uongozi wa Klabu ya Yanga umetoa pole kwa Wanachama na Mashabiki wake kutoka tawi la Kidali Asilia Tandale waliopata ajali wakiwa njiani kuelekea Morogoro ambako timu hiyo imecheza na Mtibwa Sugar na kutoka sare ya bao 1-1.
Ajali hiyo imetokea eneo la Kingorwila nje kidogo ya mji wa Morogoro imesababisha majeruhi kadhaa na uhalibifu wa mali , hivyo Uongozi umewaombea majeruhi wote wapone haraka.
Uongozi wa Yanga umesema unathamini mchango mkubwa wa Wanachama na Mashabiki katika kuisapoti timu hiyo popote inapocheza hapa nchini.


Post a Comment

0 Comments