BETI NASI UTAJIRIKE

MASHINE MBILI YANGA ZINAANDALIWA KUIMALIZA SIMBA FA


Kiungo Papii Tshishimbi amerejea rasmi mazoezin baada ya kuwa nje ya uwanja kutokana na majeraha ya mguu. Tshishimbi anaungana na beki wa zamani wa Yanga SC Mzanzibar , Abdallah Shaibu "Ninja" (21) leo jioni kwenye mazoezi pamoja na wachezaji wa kikosi cha Yanga SC jijini Dar es salaam yakiwa ni maandalizi kwa ajili ya michezo inayofuata ya Ligi kuu Tanzania Bara pamoja na kombe la Azam Sports federation Cup.

Kurejea kwa Tshishimbi na Ninja ni neema kwa Yanga wenye michezo mitatu migumu ukiwemo wa Kagera Sugar ligi kuu, Biashara United ligi kuu na ule wa nusu fainali dhidi ya watani wa jadi Simba utakaopigwa Julai 12.

Post a Comment

0 Comments