ads

adds

TETESI:HIZI HAPA MASHINE 3 ZA NAMUNGO ZINAZOPIGIWA HESABU NA AZAM FC

 
Ofisa Habari wa Azam FC Zakaria Thabit amesema kuwa kwenye dirisha la usajili watatumia ndiga yao kupaki nje ya timu ambayo watakwenda kuchukua wachezaji inaelezwa kuwa timu ya kwanza ni Namungo.
Thabit alisema kuwa kwa sasa wanachosubiri Azam FC ni ripoti ya Kocha Mkuu, Aristica Cioaba kuwataja wachezaji anaowahitaji kisha wao watashughulikia kuzipata saini zao.
“Tunasubiri kuona, Kocha Mkuu atasema anahitaji wachezaji kutoka timu ipi iwe Tanzania ama nje ya nchi, tuna gari letu kubwa la kisasa tutakachokifanya ni kwenda pale kwenye timu ambayo itapendekezwa,” amesema Thabit.
Habari kutoka ndani zinaeleza kuwa miongoni mwa wachezaji ambao wanahitajika kutoka Namungo ni pamoja na Relliats Lusajo mwenye mabao 12, Bigirimana Blaise mwenye mabao 10 na Lukas Kikoti mwenye mabao manne.
Azam FC inatatizo kwenye ushambuliaji hivyo wanahitaji kuongeza nguvu upande wa ushambuliaji na viungo hivyo miongoni mwa wanaohitajika ni pamoja na Lusajo, Kikoti na Blaise,” ilieleza taarifa hiyo.

Post a Comment

0 Comments