BETI NASI UTAJIRIKE

TETESI ZA SOKA ULAYA LEO JUMATANO TAREHE 29-07-2020


Manchester United waliandaa ofa ya kwanza ya Pauni milioni 89 ili kumpata Winga Jadon Sancho ambayo imekataliwa na Borrusia Dotmund (Bild)
Manchester United bado haijawasilisha zabuni kwa ajili ya Sancho pamoja na kwamba Dortmund inahitaji pauni milioni 110 kiasi ambacho ni kiasi kikubwa cha pesa, lakini inaaminika kuwa mazungumzo yataweza kuwafikisha kwenye makubaliano (Telegraph)
Kiungo wa Aston Villa Jack Grealish ni mchezaji anayewindwa na boss Man United Ole Gunnar Solskjaer lakini mchezaji huyo ameambiwa anatakiwa kujua hatoweza kuanza kila mchezo kila wiki ikiwa Atatua katika viunga vya Old Trafford (Independent)
Kiungo wa kati wa Leicester City James Maddison,23, amesaini dili jipya la pauni 110,000 kwa wiki ambalo litamfanya aichezee klabu hiyo mpaka mwaka 2024. (Goal)
Chelsea imeanza mazungumzo na Bayer Leverkusen kwa ajili ya Kai Havertz
Maelezo ya picha,
Chelsea imeanza mazungumzo na Bayer Leverkusen kwa ajili ya winga Mjerumani Kai Havertz, 21 (Guardian)
Winga wa Brazil Willian ,31, anaweza kukubali mkataba mpya na Chelsea mwishoni mwa wiki baada ya mazungumzo baina ya pande mbili. (Sky Sports)
Mbrazil Willian anasakwa na Chelsea
Maelezo ya picha,
Kiungo mchezeshaji anayekipiga Barcelona Philippe Coutinho ameiomba Arsenal muda zaidi kufanya maamuzi kuhusu mustakabali wake, huku Leicester City na Tottenham pia wakiwa wanamtolea macho Mbrazili huyo, 28 (Metro)
Kocha wa Bournemouth Eddie Howe atafanya mazungumzo na uongozi wa klabu saa 48 zijazo, kuhusu mustakabali wake. (Mail)
Manchester City wanajiandaa kumsajili Cameron Coxe
Maelezo ya picha,
Timu ya Ujerumani Bayern Munich wako tayari kulipa pauni milioni 18.3 kumsajili beki wa kulia wa Norwich City Max Aarons,20. (Sky Sports)
Manchester City wanajiandaa kumsajili mchezaji wa nafasi ya ulinzi wa Wales Cameron Coxe, 21 kwa uhamisho huru, baada ya kuachiwa na Cardiff City. (Wales Online)

Post a Comment

0 Comments