BETI NASI UTAJIRIKE

TETESI ZA SOKA DUNIANI LEO ALHAMIS TAREHE 17-07-2020

Kiungo Mfaransa Paul Pogba, 27 , yuko karibu kukubali mkataba mpya wa miaka mitano kuichezea Manchester United. (Sun)
Bayer Leverkusen wamekubali kuwa kiungo wa kati Mjerumani Kai Havertz, 21, amechagua kujiunga na Chelsea lakini klabu hiyo inataka kuusogeza mbele uhamisho mpaka mwishoni mwa mwezi Agosti.(Daily Star)
Beki wa kushoto wa Ajax Nicolas Tagliafico, 27,ni mchezaji muhimu kwa Manchester City msimu huu. (Sports Illustrated)
Kiungo wa Uhispania Thiago Alcantara,29, anaamini kuwa ataelekea Liverpool baada ya kukataa mkataba mpya na Bayern Munich.( Daily Mirror)

Thiago Alcantara
Arsenal iko mbioni kumsajili beki Mfaransa Malang Sarr, lakini mchezaji huyo, 21, anayepatikana kwa uhamisho wa bila malipo akitokea Nice tayari ameshafuatiliwa na vilabu vya Italia na Ujerumani.( Sun)
Manchester United imekubali kuingia mkataba na beki wa kushoto wa Real Madrid, Alvaro Fernandez Carreras, 17, ambaye atatia saini mkataba wa miaka minne kukipiga Old Trafford. (AS-in Spanish)
Kocha wa zamani wa Southampton na Tottenham Mauricio Pochettino yuko kwenye orodha ya Inter Milan na Juventus ikiwa vilabu hivyo vya Italia vitawafuta kazi makocha wa zamani wa Chelsea - Antonio Conte na Maurizio Sarri - mwishoni mwa msimu. (Daily Telegraph)

Mauricio Pochettino
Kocha wa Inter, Conte analazimika kuishawishi bodi ya klabu kukubali mshahara wa N'Golo Kante na kumsajili kiungo huyo,29, kutoka Chelsea.(SempreInter)
Kiungo wa kati Muingereza Jude Bellingham, 17, amekamilisha vipimo vya matibabu katika klabu ya Borussia Dortmund kabla ya kuondoka klabu ya Birmingham, lakini kwanza atakamilisha msimu huu na The Blues (Sky Sports)
Tottenham inaweza kumkosa mchezaji wa nafasi ya ulinzi Serge Aurier, 27, baada ya kurudi Ufaransa kutokana na kifo cha kaka yake. (Evening Standard)
Everton imetoa ofa kwa kiungo wa Napoli Allan, lakini klabu hiyo ya Italia imesitisha makubaliano na mchezaji huyo Mbrazili,29, (Sport Witness)

Serge Aurier
Kocha Roy Hodgson amesema kuwasili kwa sura mpya Crystal Palace msimu huu kutaruhusu klabu hiyo kuwa na malengo makubwa msimu ujao na kuwania nafasi 10 za juu. (Evening Standard)
Manchester City imekubaliana na masharti ya winga wa Valencia Mhispania Ferran Torres,20. (Eurosport)
Manchester United haina mpango wa kumjumuisha mchezaji wa nafasi ya ulinzi Muajentina Marcos Rojo,30, katika kikosi chao cha kwanza baada ya kukatishwa tamaa na kiwango cha mchezo wake akiichezea klabu ya Estudiantes kwa mkopo (Manchester Evening News)
Raia wa Argentina na beki wa zamani wa Italia Ezequiel Schelotto, 31, ameweka wazi kuwa anaondoka Brighton na amelenga kurejea Serie A. (The Argus)

Marcos Rojo
West Ham,Norwich na Watford zinamuwania kiungo wa kati wa QPR Ryan Manning,24. (Football Insider)
Kocha wa Leicester Brendan Rodgers anamfuatilia kwa karibu mchezaji wa Roma Amadou Diawara. Kiungo huyo wa kati anayetimiza miaka 23, Ijumaa ya leo,pia amehusishwa na Tottenham na Newcastle. (Leicester Mercury)
Walsall inaendelea kufanya mazungumzo na kiungo wa England Danny Guthrie ,33, kuhusu mkataba mpya. (Express & Star)

Post a Comment

0 Comments