BETI NASI UTAJIRIKE

TETESI ZA SOKA DUNIANI LEO JUMATANO TAREHE 08-07-2020


Mkufunzi wa Chelsea Frank Lampard amemlenga kiungo wa kati wa West Ham na England Declan Rice, 21, kama kiungo muhimu wa kikosi chake.(Times - subscription required)
Manchester City na Manchester United zote zinawanyatia mabeki wawili tofauti huku beki wa Napoli na Senegal Kalidou Koulibaly,29, na beki mwenye umri wa miaka 25 Milan Skriniar, anayeichezea Inter Milan na Sloviakia, wakilengwa . (Independent)
Chelsea na Real Madrid zote zimeimarisha juhudi zao kumsaini kiungo wa kati wa Lazio Sergej Milinkovic - Savic huku wakijaribu kuwa kifua mbele kuzipiku klabu za Man United na PSG kupata saini ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 raia wa Serbia. (Gazzetta dello Sport, via Express)
Sergej Milinkovic
Maelezo ya picha,
Mkufunzi wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer alimwambia beki wa kati wa Bournemouth Nathan Ake kwamba tunahitaji beki wa mguu wa kushoto, hivyobasi akamwambia endelea kuimarika baada ya kukamilika kwa mechi ambayo Bournemouth ilioteza 5-2 katika uwanja wa Old Trafford siku ya Jumamosi. (Telegraph)
Crystal Palace inapanga uhamisho wa dau la £25m kumnunua mshambuliaji wa Celtic na Ufaransa Odsonne Edouard, 22. (Sun)
Bayern Munich itamwacha beki wa Austria 28, David Alaba, ambaye kandarasi yake inakamilika 2021, kuamua iwapo anataka kusalia na klabu hiyo ama kuhamia katika ligi ya Premia. (Mirror)
Odsonne Edouard
Maelezo ya picha,
Crystal Palace kumnunua mshambuliaji wa Celtic na Ufaransa Odsonne Edouard
RB Leipzig inataraji kwamba beki wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 21 Dayot Upamecano, ambaye amehusishwa na uhamisho wa Arsenal , ataongeza kandarasi yake baada ya kukamilika 2021. (Mirror)
Juventus inataka kumsaini kiungo wa kati wa Chelsea na Italy Jorginho, 28 mwisho wa msimu huu. (Tuttosport, via Sun)
Real Madrid haina mpango wa kumsajili mchezaji yeyote mwisho wa msimu huu kutokana na athari za mlipuko wa corona. Badala yake , klabu hiyo inatumai itachangisha £190m kupitia uuzaji wa wachezaji huku winga Gareth Bale, 30, akihusishwa na uhamisho. (Marca, via Star)
Gareth Bale
Maelezo ya picha,
Mkufunzi wa Real Madrid Zinedine Zidane alichangia kwa mchezaji wa Morocco Achraf Hakimi, 21, kuondoka katika klabu hiyo ya Uhipsnia ili kujiunga na Inter Milan, kulingana na wakala wa beki huyo. (Marca)
Beki wa zamani wa England John Terry, ambaye ni naibu wa kocha wa klabu ya Aston Villa Dean Smith, anatarajiwa kuwa mkufunzi mpya wa klabu ya ligi ya mabingwa Bristol City. (Football Insider)

Post a Comment

0 Comments